Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Mhe. Dkt. Pindi Chana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mkiwa baada ya sikuchache kuvamiwa na Tembo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akimkaribisha Waziri wa Maliasili baada ya kufika katika eneo hilo.
IKUNGI
Na Mwandishi Wetu
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mkiwa, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wameiomba serikali kuwapatia mafunzo maalumu ya vijana wa kijiji hicho ili waweze kukabiliana na changamoto ya tembo waharibifu katika maeneo yao.
Ombi hilo limetolewa leo tarehe 28 Oktoba 2024, wakati wa mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Mhe. Dkt. Pindi Chana, na wananchi wa Mkiwa, kufuatia tukio la tembo kuharibu mazao na makazi katika baadhi ya maeneo ya kijiji hicho ambacho pia ni njia ya tembo.
Waziri Dkt. Chana ameagiza hatua kadhaa kuchukuliwa ikiwemo kutambua na kuhifadhi korido za tembo kwa kushirikiana na wananchi, kuongeza askari wa wanyamapori, kutoa elimu kwa wananchi, na kuongeza vifaa maalumu vya kudhibiti na kuswaga tembo kuelekea maeneo ya hifadhi.
Aidha, amepongeza juhudi za serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha wizara ya Maliasili na Utalii ili kuhakikisha wanyamapori wanalindwa bila kuathiri miundombinu na mazao ya wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Apson, ameipongeza wizara hiyo kwa kujitokeza kutatua changamoto hiyo.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Kati, Ndg.
Herman Nyanda, amesema askari wanne wa Wilaya ya Ikungi na wengine 15 wa Mkoa
wa Singida wamepewa mafunzo maalumu ya kukabiliana na wanyama pori waharibifu.
0 Comments