Na Mwandishi wetu - Mkalama
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses
Machali amepiga marufuku kwa wafanyabiashara pamoja na wakulima wilayani
Mkalama kuuza na kununua zao la Dengu
nje ya mfumo wa Stakabadhi Ghalani.
Marufuku hiyo ameitoa Agosti 13,2024
wakati wa mnada wa kwanza wa Dengu uliofanyika katika ghala la mazao lililopo
Nduguti kwa njia ya mfumo wa TMX ambao umeshuhudia bei kwa kilo ikiuzwa kwa
shilingi 2003.282
“Lengo la serikali ni kumnyanyua
Mkulima, tunaka Mkulima auze Dengu yake hapa, hivyo kuanzia leo napiga marufuku
kwa mtu yeyote kununua na kuuza Dengu shambani, atakayebainika atachukuliwa
hatua kali za kinidhamu” Mhe. Machali
Mhe. Moses Machali pia amepiga
marufuku kwa wafanyabiashara kusafirisha zao la Dengu nyakati za usiku bila ya
kibali kinachoonesha Dengu hiyo imenunuliwa katika Ghala “kuanzia leo marufuku kusafirisha Dengu
wakati wa usiku Kwenda wilaya nyingine ikiwa hauna kibali maalumu, natoa siku
saba kwa wafanyabiashara ambao walikuwa tayari wamenunua Dengu walete hapa
Ghalani.” Mhe. Machali
Aidha Mhe. Moses Machali amewataka
wakulima wilayani Mkalama kuzingatia kanuni za kilimo bora kwa kutumia mbolea
kwa wingi ili waweze kupata mazao mengi na kupelekea kukuza Uchumi wao.
“Serikali ya awamu ya sita imedhamiria
kunyanyua sekta ya kilimo nchini, nawasihi wakulima nendeni mkajindikishe,
serikali ipo kwa ajili yako Mkulima, tumieni fursa hii vizuri” Mhe. Machali
0 Comments