TAARIFA KUHUSU UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO NA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA YA MANISPAA YA SINGIDA


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mhe, Yagi Kiaratu akiongozana na kamati ya Fedha na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida katika zoezi la Ukaguzi wa Miradi hiyo ya Maendeleo.



Na Mwandishi Wetu

Leo, Novemba 7, 2024, Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida imekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa maelekezo kwa Menejimenti ya Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ubora na viwango vya juu.

Kamati hiyo, inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Mhe. Yagi Kiaratu, ilifanya ziara ya ukaguzi na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa miradi kwa ufanisi na kwa wakati.

Meya Kiaratu alisisitiza kwamba miradi hiyo lazima ikamilike kwa ubora wa juu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa sita na matundu nane ya vyoo katika Shule ya Sekondari ya Mandewa, ambayo imekamilika. Kamati pia ilitembelea ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mwaja, inayojengwa katika Kata ya Mandewa, na ilikagua miundombinu ya kidato cha tano na sita katika Sekondari ya Mufumbu, ikiwa katika hatua ya umaliziaji kwa upande wa madarasa na mabweni yakiwa katika hatua za awali.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

1 Comments