Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ameelezea masikitiko yake makubwa kuhusu tukio lililotokea katika Kata ya Ntuntu, Wilaya ya Ikungi. Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida, ambayo yeye ni mwenyekiti, Dendego alilaani vikali kitendo hicho.
Kwa mujibu wa Dendego, Diwani wa Kata ya Ntuntu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Omary Nkonki Toto, pamoja na wafuasi wake 13, walimvamia Mtendaji wa Kijiji cha Ntewa “A”, Ramadhani Idi Nyengo, kinyume na sheria na taratibu za nchi.
“Kitendo hiki cha hovyo hakiwezi kukubalika mbele ya jamii,” alisema Dendego. Aliagiza vyombo vya dola kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja.
0 Comments