HALMASHAURI YA IKUNGI YAKUSANYA ZAIDI YA ASILIMIA 114 YA MAPATO.

Mkurugenzi wa Halmashauri Justice Kijazi amewataka madiwani kubunu miradi ili kuongeza mapato ya halmashauri.


Mwenyekiti wa halmashauri amewataka maafisa ughani kuhakikisha wanaongeza juhudi katika mazao ya biasahara.


Katibu Tawala Msaidi wa serikali za mitaa mkoa wa Singida Shaban Mongomogo ameipongeza halmashauri ya Ikungi kwa ukusanyaji mzuri wa mapato.


Madiwani wa kata mbalimbali wakisoma taarifa za mapato na matumizi akiwemo diwani wa kata ya Mang"onnyi Mhe. Innocent Makomelo 



 Na Mwandishi watu -Ikungi

  Inaelezwa kuwa kiasi cha makusanyo ya mapato ya Halmashauri ya wilaya ya singida mpaka sasa kimefikia zaidi ya asilimia 114 mpaka sasa.

Baadhi ya madiwani waomba maafisa kilimo Wilaya ya Ikungi kufanya utafiti katika kila kata hasa zinazofanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato ili kujua aina ya mazao yanayopaswa kulimwa katika Kata hizo kuongeza mapato ya Halmashauri.

Hayo yamesemwa hii leo katika kikao cha baraza la madiwani la kujadili taarifa za mapato ya Halmashauri hii leo tarehe 21 Agosti, 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri lengo ikiwa ni kuongeza ukusanyaji wa mapato na kukuza maendeleo wilayani hapa.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe. Ally Juma Mwanga amepongeza baadhi ya kata zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwani mapato ndio kitovu cha maendeleo ya Halmashauri na kuwaomba waliofanya vibaya kujitahidi kudhibiti mianya ya utoroshaji wa mazao nyakati za usiku.

"Halmashauri kukusanya mapato zaidi ya asilimia 114 ni hatua nzuri sana na naomba tuendelee hivyo ili kuvuka malengo zaidi" amezungumza" Mhe Mwanga.

Wajumbe wa kikao hicho wameongeza na kusema kuwa Kuna umuhimu wa Kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kutokutegemea vyanzo vya msimu wa kilimo pekee mfano minada, vivutio mbalimbali, pamoja na vibanda vya biashara katika maeneo kama vituo vya mabasi hii itaongeza ukusanyaji wa mapato yakudumu na hatimaye kujikwamua kiuchumi na kutoa fursa kwa wananchi kuongeza kipato kupitia ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi awataka watendaji wa Kata na vijiji kushirikiana kwa karibu ili kukusanya mapato ya Halmashauri kikamilifu na kuziba mianya ya utoroshaji wa mazao katika maeneo korofi.

"Tupo tayari kutoa motisha kwa Kata zinazofanya vizuri ukusanyaji wa mapato ili kuhamasisha ukusanyaji kata zinazofanya vibaya nao kufanya vizuri zaidi" amezungumza Kijazi

Kikao hicho cha baraza la madiwani kimehudhuriwa na Kamati ya ulinzi na usalama, madiwani, viongozi wa dini watendaji wa Kata na wawakikishi wa watendaji wa vijiji wazee, pamoja na wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya
ya Ikungi

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments