Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki
Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds
Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa
imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith
Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.
Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai
Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka
huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.
Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba
mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni
kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru aombe
radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara ya jumla kwa
jinsi mahakama itakavyoona inafaa.
Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye
baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea
nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”
Wakati akijibu shitaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee
wa upande wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama imemtaka aombe radhi
kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa nchini na ikiwezekana
duniani pia
0 Comments