MASHIRIKA NA TAASISI BINAFSI YATAKIWA KUTIMIZA MALENGO WALIYOJIWEKEA.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego katika mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Mkoa wa Singida.

Happy Frances Mwenyekiti wa umoja wa Mashirika hayo akiongea katika mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa RC MISION Singida Mjini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sema Singida Ivo Manyaku akiongea katika mkutano huo.



Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya wasaidizi wa kisheria SLAP Theresia Mande akimuelezea mgeni rasimi Mkuu wa wilaya ya Singida Thjomas Apson juu ya shughuli zao za kila siku.

Singida

23.08.2024

Mashirika yasiyo ya kiserikali yametakiwa  kufanya kazi zao kwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwa mashirika hayo ili kuepuka kufutiwa usajili wa mashirika hayo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas Apson akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego katika jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Singida lililofanyika katika ukumbi wa RC Mission mjini hapo.

Amesema ni vizuri mashirika hayo kufanya kazi kwa weledi na kusimama kwa miguu yao wenyewe na sio kutegemea wafadhili ambao pengine wanaweza kutoa fedha kwa masharti magumu huku mengine yakapelekea kuvunjwa kwa maadili na tamaduni za jamii na nchi kwa ujumla.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika la Sustainable and Environment Management Action - SEMA ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wadau wa mashirika hayo kutuma taarifa zao za kazi kwenye mfumo na kwa msajili.

Awali akisoma taarifa ya mashirika hayo mjumbe wa National Council of NGO’s - NACONGO Mkoa wa Singida na mjumbe wa bodi hiyo Taifa Happyness Mwasenga amesema mashirika yasiyo ya kiserikali yamekua yakisaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali katika jamii.

Kauli mbiu katika maadhimisho ya jukwaa hilo ni Mashirika yasiyo ya kiserikali ni wadau muhimu, washirikishwe kuimarisha utawala bora.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments