Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Asiya Messo akitoa maelezo baada ya mnada wa zao hilo uliyotumia jia ya kidigitali kumalizika.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Moses Machali akitoa maelekezo kwa wakulima na wanunuzi wa zao la Dengu juu ya mfumo wa manunuzi.
SNGIDA
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali amepiga marufuku kwa
wafanyabiashara pamoja na wakulima wilayani Mkalama kuuza na
kununua zao la Dengu nje ya mfumo wa Stakabadhi Ghalani.
Marufuku hiyo ameitoa wakati wa mnada wa kwanza wa Dengu
uliofanyika katika ghala la mazao lililopo Nduguti kwa njia ya mfumo wa TMX
ambao umeshuhudia bei kwa kilo ikiuzwa kwa shilingi 2003.282
Mhe. Moses Machali pia amepiga marufuku kwa wafanyabiashara
kusafirisha zao la Dengu nyakati za usiku bila ya kibali kinachoonesha Dengu
hiyo imenunuliwa katika Ghala.
Aidha Mhe. Moses Machali amewataka wakulima wilayani Mkalama
kuzingatia kanuni za kilimo bora kwa kutumia mbolea kwa wingi ili waweze kupata
mazao mengi na kupelekea kukuza Uchumi wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkalama Asia Messos amewataka wakulima wilayani Mkalama kutumia mfumo wa
Stakabadhi Ghalani ili kunufaika kwa kuuza mazao kwa bei inayoendana na soko.
0 Comments