Ikungi
Alhamisi 15 Augusti, 2024
MWANAFUNZI mmoja wa Shule ya
Msingi Italala Kijiji cha Musimi kata ya Sepuka Wilaya ya ikungi mkoani Singida
Faidhati Juma (7) anayesoma darasa la kwanza amekufa kwa kutumbukia kisimani
akichota maji akiwa na wenzake.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa na Mwenyeiti wa Kijiji cha Musimi Omari Soa zinasema mwanafunzi
huyo amekufa maji baada ya kudaiwa aliteleza juu ya kingo za kisima chenye
urefu wa mita sita na kutumbukia ndani ya maji akitanguliza kichwa saa 11:00
jioni akiwa na wenzake.
Mwenyekiti Omari amesema baada ya
mwanfunzi huyo kutumbukia kisimani na kuzama ndani akiwa amevaa nguo za shule,
baada ya wenzake kuona hali hiyo wakakimbia haraka nyumbani huku wakilia nakutoa
taarifa kwa mama yake Adija Athumani kwamba mwenzao
Faidhati ametumbukia kisimani na
galoni lake wakati anachota maji na hakutokeza juu.
Mama yake alipopata habari hizo akatoka
mbio huku akilia akaenda kisimani akiongozana na Watoto wenzake waliotoa
taarifa majirani, ndugu jamaa na watu wengine wakamfuata mpaka kisimani nakumkuta Faidhati tayari amepoteza
Maisha akiwa anaelea juu ya maji wakatoa taarifa kwa viongozi wa Kijiji na
Polisi wa kituo cha Sepuka.
Imeelezwa katika kikao cha
dharura hapo kisimani akiwepo Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Italala Magharibi Hamisi Kitwanga na wazazi wa mtoto huyo
pamoja na majirani na ndugu waliofika kushuhudia tukio hilo waliamua kumtoa
kisimani mtoto huyo na kumpeleka nyumbani.
Polisi wa Kituo cha Sepuka
walifika katika kisima hicho wakifuatana na Mganga wa Kituo cha Afya Sepuka
kushuhudia, uchunguzi na maelezo mengine katika taarifa yao wamesema mwanafunzi
huyo alifika kisimani hapo kwa lengo la kuchota maji, hakuna jingine kwenye
tukio hilo ni jambo la kawaida kutokea katika jamii , hivyo taratibu zingine za
maziko yake yafanyike kwa mujibu wa dini yake.
Akitoa salamu za Serikali katika
mazishi ya mwanafunzi huyo Diwani wa kata ya Sepuka Halima Ng’imba amesema
taifa, shule na wazazi wamepoteza mtu muhimu sana katika nchi hii kwani baadae
angekuja kuwa kiongozi, hivyo jamii yote ina masikitiko makubwa kwa kumkosa
Faidhati na serikali inatoa pole kwa jamii yote.
Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu
wa Shule ya Msingi italala Linus Msaky amesema mwanafunzi huyo alikuwa ana bidii
katika masomo yake na alikuwa ana mahudhurio mazuri shuleni, mtulivu na
mahusiano mazuri na wenzake, hivyo Walimu na Wanafunzi wenzake wanamasikitiko
makubwa kwa kumkosa Faidhati.
Imamu wa Msikiti Mkuu wa Sepuka
Sheikh Juma Malali aliyeongoza mazishi hayo katika hotuba yake amesema hii ni
kazi ya Mung una Msikiti unatoa pole kwa walimu, wazazi, ndugu na jamii yote na
wote tunakumbushwa kumuabudu Mung una ndiyo hasa malengo ya kutuumba sisi
wanadamu na kutuweka hapa duniani.
Amesema “Mungu kweli ametuumba
sisi lakini ametuficha sana vitu vitatu katika Maisha yetu siku ya kuzaliwa,
riziki atakazopata mt una siku ya kufa katika siku hizo tatu au vitu hivyo
vitatu hakuna anayejua ni Mung utu ndiye anayejua pekee yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida
Amon Kakwale amesema katika tukio hilo hakuna shaka la kosa la jinai ni la
kawaida kutokea katika jamii kufanyika hivyo jamii ishiriki mazishi yake kwa mujibu
wa dini yake.
0 Comments