Na Mwandishi wetu Singida
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amewaagiza Maafisa Madini waliopo katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wanawatambua wachimbaji wadogo wa madini na kuwaelekeza mbinu bora za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.
Utekelezaji huo, inaelezwa kuwa ni moja ya jukumu la Wizara la kuhakikisha inawatambua na kuwarasimisha wachimbaji wadogo wa madini ili wachimbe kwa faida na watoke kwenye uchimbaji mdogo waende wa kati na hatimaye kwenye uchimbaji mkubwa.
Hayo yamebainishwa na Dkt. Kiruswa alikuwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Singida ambapo amesema Wizara yake inaendelea na jitihada za kuwatambua na kuwarasimisha wachimbaji wadogo wa madini kote nchini.
"Naomba nichukue fursa hii kuwataka watumishi wote wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi yaa Mkoa wa Singida kuwa wabunifu katika utendaji kazi wenu ili muweze kuwasadia wachimbaji wa Mkoa huu na kutafuta njia rafiki za ukusanyaji wa maduhuli ya serikali," amesema Dkt. Kiruswa.
wananchi wakimsikiliza naibu wazari wakatati wa mkutano huo uliyofanyika Mkoani Singida .
Aidha, Dkt. Kiruswa amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo kuhakikisha wanakutana kabla ya Januari 30, 2022 ili kujadili namna ya kuutatua mgogoro wa wachimbaji wadogo wa eneo la Mkombozi ulio dumu kwa muda mrefu.
Chone amemuahidi Dkt. Kiruswa kuyafanyia kazi maagizo yake yote aliyoyatoa mkoani humo na kumuelezea changamoto ya upungufu wa watumishi pamoja na vitendea kazi inayo ikabili ofisi yake.



0 Comments