DRC YATISHIA VYOMBO VYA HABARI

Waziri wa Habari Lambert Mende
Umoja wa Mataifa unasema kuwa kuna wasi wasi kufuatia sheria mpya nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ambayo inavitaka vituo vya habari vya kigeni kujiandikisha kama makampuni ya nchi hiyo la sivyo matangazo yao yazimwe.

Sheria hizo mpya zitaanza kutekelezwa mwishoni mwa wiki hii.
Vyombo vya habari vya kigeni sasa vitaruhusiwa kutangaza nchini DRC, ikiwa asilimia kubwa ya wenye hisa mi raia wa Congo.

Maafisa wamevipa vyombo hivyo muda wa siku 30 kutekeleza matakwa hayo
Sheria hizo zinaathiri vitua kama Radio France Kimataifa(RFI) Sauti ya Amerika na BBC.


Matangazo ya RFI kwa sasa yamezimwa nchinin DRC, tangu itangaze mipango ya upinzani ya kufanya maandamano mapema mwezi ujao.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments