mkuu wa mkoa wa Singida Eng Methew Mtigumwe akiongea na wananchi wa ilongero pembeni yake ni mkuu wa wilaya ya Singida. |
M/kiti wa CCM mkoa wa Singida Matha Mlata akitoa maagizo ya ofisi za chama kuamia Ilongero. |
Mbunge wa Jimbo Lazaro Nyalandu |
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe
amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Singida kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya
kuhamishia makao makuu ya halmashauri ya Singida katika mji mdogo wa Ilongero
ndani ya kipindi cha miezi sita ili kusogeza huduma karibu na wananchi wa
halmashauri hiyo.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amefikia uamuzi huo kutokana na taarifa za
kuwepo watu wachache wanaotaka kufanya mabadiliko ya makao makuu bila ya
kusikiliza mawazo ya wananchi wengi huku wananchi wakipendelea makao makuu ya
halmashauri hiyo kuwa katika mji mdogo wa Ilongero.
Ameongeza kuwa baraza la madiwani la halmashauri ya Singida linapaswa
kuketi tena na kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya wananchi wengi huku
akiongeza kuwa endapo wanataka kufanya mabadiliko wayafanye wakiwa tayari
wameshahamia katika halmashauri yao tofauti na sasa ambapo bado ofisi zipo
manispaa ya Singida.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amesema wananchi wanataka kupatiwa huduma
kwa ukaribu hivyo halmashauri kuhamishiwa Ilongero itasaidia kusogeza Huduma
ambapo zitatolewa kwa ufanisi huku akimshauri Mkurugenzi wa halmashauri hiyo
kujipanga ndani ya kipindi hicho waanze kutumia ofisi chache zilizopo.
Aidha Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amewataka wananchi wa halmashauri na
Mkoa mzima wa Singida kujituma na kufanya kazi kwa bidii, wakulima wajiandae
FEMA kwa msimu huu wa kilimo na kujitahidi kutunza vyakula ili kujiepusha na
njaa na wafanyabiashara watumie fursa mbalimbali kujiongezea kipato.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Martha
Mlata amesema chama hicho mkono mapendekezo ya wananchi yakutaka makao
makuu kuwa katika mji mdogo wa Ilongero na kuahidi kufuatilia na kusimamia
utekelezaji wake.
Katika kuunga mkono mapendekezo ya wananchi Mbunge wa jumbo la Singida
kaskazini la kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu amesema kufikia mwezi Januari
ataweka ofisi za Mbunge katika mji wa ili wananchi wapate Huduma na kumfikishia
kero kwa ukaribu zaidi.
0 Comments