Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi
Mathew John Mtigumwe akipata maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto
mahututi (Neonatal Intensive care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani
Iramba.
Mkurugenzi wa Shirika la Water Aid Tanzania uu
wa Dokta Ibrahim Kabole akipata maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto
mahututi (Neonatal Intensive care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani
Iramba.
Mwakilishi wa Shirika la Water Aid
International akiangalia akinamama wanaosubiri kujifungua wakichota maji,
miundombinu ya maji imekarabatiwa na shirika hilo wakishirikiana na shirika la
SEMA Tanzania.
Mwakilishi wa Shirika la Water Aid
International akipata maelezo kuhusu kitengo cha huduma ya watoto mahututi
(Neonatal Intensive care unit) katika hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba,
pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dokta Boniphace Richard.
Matenki ya maji yaliyokarabatiwa na Shirika la Water Aid International kwa ushirikiano na shirika la SEMA Tanzania. |
Akina mama wanaosubiria kujifungua
wakiwa nje ya wodi ya kusubiria iliyokarabatiwa kwa ufadhili wa shirika la
Water Aid wakishirikiana na shirika la SEMA Tanzania.
|
Jengo la mbele ni Kichomea taka cha
zamani na nyuma yake ni jengo jeupe jipya ni kichomea taka kipya na cha kisasa
kilichojengwa na Shirika la Water Aid International kwa ushirikiano na shirika
la SEMA Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe
ameipongeza hospitali ya Kiomboi ambayo ni ya Wilaya ya Iramba kwa kupata hadhi
ya nyota mbili kutoka sifuri na kuwahamasisha kuendelea kuboresha utendaji ili
kupata hadhi ya nyota tatu.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ametoa pongezi hizo alipotembelea
hospitali hiyo akiambatana na wageni kutoka shirika la Water Aid International
ambalo limefadhili ukarabati wa miundombinu hospitalini hapo kwa shilingi
milioni mia tano kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amesema hospitali ikiwa na hadhi ya nyota tatu itasaidiwa na
serikali pamoja na wadau mbalimbali katika kuipatia wataalamu zaidi,
kuboreshewa zaidi miundombinu, kuwekwa katika mipango ya kitaifa pamoja na
kupata fedha zaidi.
Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa kutokana na kuboreka
kwa huduma za hospitali ya Kiomboi wagonjwa wameongezeka sana na hivyo ofisi ya
Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri ya Wilaya ya Iramba inaboresha
Vituo vya Afya vya Mgongo na Ndago ili vituo huduma za zarudha za Mama na
mototo kwa kufanya upasuaji na hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa katika
hospitali ya Kiomboi.
Naye Mkurugenzi wa shirika la Water Aid Tanzania Dokta Ibrahim
Kabole ameshukuru ushirikiano wanaoupata kutoka kwa watendaji wa wilaya ya
Kiomboi hadi kufanikisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya hospitali ya
Kiomboi huku akiwataka kuitunza na kuendeleza pale shirika hilo lilipoishia.
Dokta Kabole amesema shirika hilo limekarabati wodi ya wazazi
wanaosubiria kujifungua, kuweka miundombinu ya maji na matenki, kujenga
kichomea taka kipya chenye hadi ya kisasa hospitalini hapo, kununua friji ya
kuhifadhia damu katika kituo cha acya cha ndago na kutoa mafunzo kwa watoa
huduma.
Ameongeza kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na viongozi
wa Mkoa wa Singida katika kuboresha sekta ya afya mkoani hapa hasa katika
kuboresha afya ya mama na mtoto.
Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kiomboi Dokta Boniphace Richard
ameishukuru Water Aid na kuongeza kuwa imesaidia hospitali hiyo kupata hadhi ya
nyota mbili kutoka sifuri kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya hospitali
hiyo.
Dokta Richard amesema Wodi iliyoboreshwa na shirika hilo kwa
sasa inapokea wakina mama wanaosubiria kujifungua 50 ambapo awali walikuwa wana
uwezo wa kulaza 30 kwa siku, maji yanahifadhiwa lita 4500 ambazo zinasadia
akina mama hao pamoja na uendeshaji wa shughuli nyingine za hospitalini hapo,
kupungua kwa vifo vya akina mama kwa asilimia 30.
Ameongeza kuwa uboreshaji wa miundombinu hospitalini hapo
kumepelekea kuanzishwa kwa kitengo cha Watoto mahututi katika wodi ya wazazi
(Neonatal Intensive care unit), ambapo watoto wanaozaliwa na matatizo
mbalimbali wanapatiwa huduma hapo na kuokolewa maisha tofauti na awali.
0 Comments