TARURA SINGIDA DC KUTUMIA ZAIDI YA BILION MBILI 2022/2023


WAKALA wa barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya matengenezo na ujenzi wa barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2026. 

Mpango wa bajeti hiyo ya matengenezo na ujenzi wa barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2026 utahusisha mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 811.68 ambazo tayari zimeingizwa kwenye mfumo.

Akiwasilisha mpango huo wa bajeti kwenye  baraza maalumu la madiwani Halmashauri ya Singida kaimu Meneja wa Wakala huo Wilaya Mhandisi Christopher Njalika alisema jumla ya shilingi bilioni 2,201,233,784 zimetengwa kujenga mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 811.68 katika Halmashauri hiyo.

Mhandisi Njalika alisema kati ya kilomita 811.68, kilomita 439.75 ni barabara za kiwango cha changarawe,kilomita 592.63 ni kiwango cha udongo, huku kilomita 1.5 ni kiwango cha lami ambayo itajengwa katika mji wa Ilongero.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Elia Digha alitumia fursa hiyo kuupongeza Serikali kwa kuipatia fedha Halmashauri kwa ajili ya miundombinu ili wananchi waweze kufanya shughuli za kila wakati zitakazowaingizia kipatao chao na taifa kwa ujumla,huku akiwaomba Tarura Wilaya katika bajeti nyingine kuomba fedha zaidi ya hiyo kutokana na ukubwa wa Halmashauri hiyo.

Aidha aliwaomba Madiwani kwenda kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao,akitaja miradi mojawapo ni ujenzi wa maabara katika baadhi ya shule,umaliziaji wa jengo la Halmashauri pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana inayotarajiwa kujengwa katika kata ya Kinyeto.

Aliwaagiza madiwani hao kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa,na kwamba wasijihusishe wala kutajwa kuhusika kwa kukwamisha miradi hiyo.

Naye kaimu Katibu tawala Wilaya Ally Mwendo aliupongeza Wakala huo kwa kuyatambua maeneo ambayo yalikuwa hayapitiki kabisa msimu wa Mvua hali iliyokuwa inasababisha wananchi kushindwa kuendesha shughuli zao za kila siku.

"Barabara ndio uchumi,kama hakuna barabara sehemu yoyote hakuna uchumi,kila mtu anategemea barabara..niwaombe madiwani nyie mko Kila mahali pelekeni ujumbe huu kwa wananchi wenu kwamba watunze miundombinu hii ili iendelee kutusaidia." alisema Mwendo.

                                     

                                     Mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa kata ya Msange MheElia                             Digha akifunga kikoa cha baraza kilicho fanyika katika mji mdogo wa Ilongero .                                            

                                                 

              

 
 
 kaimu Meneja wa Wakala  Wilaya Mhandisi Christopher Njalika  akiwasilisha bajeti ya Tarura mbele ya baraza la madiwani.


madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida DC wakifuatilia kwa makini katika kikao hicho kilichofanyika katika Irongelo.

               viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wakifuatilia kikao hicho.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments