Na Nathaniel Limu.
BARAZA la
madiwani halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni,limepitisha kwa kauli moja
mapendekezo ya mpango wa bajeti ya metengenezo ya barabara na
madaraja, zaidi ya shilingi bilioni 2.1 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Kaimu meneja TARURA
wilaya ya Manyoni Injinia Yose Mushi,amesema mategenezo ya barabara na madaraja
kwa halmashauri ya Itigi,yatasimamiwa na wakala wa barabara vijijini
na mjini,TARURA.
Aidha,ametaja vyanzo vya
mapato kuwa ni pamoja na mfuko wa barabara zaidi ya
shilingi 638.9,fedha za jimbo shilingi milioni 500, na tozo ya mafuta shilingi
bilioni moja.
Kuhusu
matengenezo,aliyataja kuwa ni pamoja na matengenezo ya
kawaida ya urefu wa kilometa 61.96, kuimarisha sehemu korofi 5.10 na
matengenezo ya muda maalumu kilometa 3.92.Na ujenzi
wa barabara kiwango cha lami,cha kilometa moja.Pingi
hicho,wanatarajia kufunguzi barabara mpya”,alisema.
Mushi ameongeza kwamba
kazi nyingine ni ujenzi wa madaraja/makarabati /drift kilometa 24.Fedha zingine
zaidi ya shilingi 83 milioni zitatumika katika shughuli za usimaminizi. Kazi ya
upembuzi yakinifu,shilingi milioni tano,zinatarajiwa kutumika.
Baada ya kusomwa kwa
bajeti hiyo,diwani wa kata ya Itigi (CCM) Alli Minja,alisimama na kuliomba
baraza hilo maalum, lipitishe bajeti hiyo bila kupinga.Kwa madai imegusa kila
eneo katika halmashauri hiyo changa.
Aidha,Minja alitumia
fursa hiyo kuipongeza na kuishukru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais
Samia, kwa kuiongezea halmashauri hiyo fedha za kutosha, mahitaji ya
halmashauri ya Itingi katika sekta zote ikiwemo ya sekta ya barabara.
“Naiomba serikali yetu
sikivu,iendelee kuongeza fedha ili barabara nyingi iweze kuboreshwa
zaidi.TARURA nayo naiomba itoe kipaumbele barabara za pembezoni,kwa kuzifanyia
uboreshaji ili wakulima waweze kusafirisha mazao yao, bila usumbufu wa aina ye
yote”,amesema diwani Minja.
Naye mbunge wa jimbo la
Manyoni magharibi,Yahaya Omary Massare,alisema ameiunga mkono bajeti hiyo,
akidai imegusa kila eneo katika barabara za jimbo hilo.
“Binafsi nitumie muda
huu kuwapongeza watendaji wa TARURA.Kwanza kwa usikivu na
uwajibikaji wao.Injinia Ogati,hongera sana.Kwa kipindi cha awamu
yangu ya ubunge,umekuwa mshauri wangu mzuri mno, wakati wote na hata
usiku”,amesema mbunge huyo.
Naye mwenyekiti wa CCM
halmashauri ya Itigi,Jumanne Ismael,ameutaka uongozi wa halmashauri hiyo
kuongeza zaidi vyanzo vya ndani vya mapato,ili iweze kuondokana na utegemezi.
“Kwa ujumla halmashauri
yetu ya Itigi,imefanya juhudi kubwa katika kutekeleza ahadi zilizopo kwenye
ilani ya uchanguzi.Kwa njia hii,mtakuwa mmetupunguzia mno, uwezekano
wa sisi kuja kupingwa maswali umiza,katika uchaguzi mkuu
ujao”,alisema.
Akiijengea nguvu hoja yake,alisema halmashauri imefika wakati ianze kuona aibu kila mwaka kutangaza kuwa wameletea kiasi fulani na serikali au wadau wengine.Waongeze bidii kubuni na kusimamia vizuri makusanyo yao, ya ndani.
Eng.Yose Mushi,akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya
kusomwa kwa bajeti ya 2022/2023 mbele ya kikao maalum cha madiwani wa
halmashauri ya Itigi,ili kuipitisha.Bajeti hiyo ilipita bila ya kupingwa.



0 Comments