Kufuatia Kocha wa Simba,
Mbelgiji, Patrick Aussems kufukuzwa kazi jana ikiwa mkataba wake wa mwaka mmoja
haujamalizika, baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wapendekeza mdabala wake
ambaye anafaa kuchukua nafasi hiyo.
Licha ya kufutwa kazi,
baadhi wamepingana na maamuzi hayo wakiamini Aussems alikuwa ni chaguo sahihi
kuendelea na kazi hiyo kutokana na mafanikio aliyoipatia kwa muda ambao
amefanya kazi.
Wengi wao wameleeza kuwa
Simba kwa sasa inapaswa kuwa makini katika chaguo la mbadala wake sababu ipo
kwenye harakati za kutetea ubingwa wa ligi kuu bara.
Aidha, wamependekeza awe
mabala abaye atahakikisha anakuwa na uwezi juu ya Aussems ili aje aiwezeshe
kufanya vema zaidi kunako mashindano ya kimataifa.
Ikumbukwe moja ya rekodi alizoziweka Aussems ni kuchukua ubingwa
wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo sabamba na kufika kunako hatua ya robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 Comments