Mtoto wa Weah akikabidhiwa jezi ya PSG mblele ya baba yake. |
Tomothy Weah
amefuata nyayo za babake ambaye ni mshindi wa taji la Ballon d'Or George Weah
baada ya kutia saini kandarasi na klabu ya Paris St- Germain.
Mshambuliaji huyo wa miaka 17 ametia saini
mkataba wa miaka 3 na PSG klabu ambayo George Weah aliiwakilisha kutoka mwaka
1992 hadi 1995.
Tayari kumekuwa na uvumi kwamba mwana
anafuata nyayo za babake.
Mnamo mwezi Septemba 2016, kinda Weah
alifunga hat-trick katika ushindi wa 8-1 dhidi ya klabu ya Ludogorets katika
mechi yake ya kwanza ya Uefa.
''Ni fahari kubwa kuendeleza pale baba
alipowachia'' , alisema Weah ambaye alizaliwa mjini New York na kujiunga na New
York Red Bulls kabla ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya soka cha PSG mnamo
mwezi Julai 2014.
''Niko katika klabu kubwa na natumai
nitaendelea kuimarika ili niweze kuichezea timu kubwa''.
Weah katika fainali mwaka 2000 FA CUP na chersea |
Babake mwenye umri wa miaka 50 kutoka Liberia
aliwahi kushinda mara tatu taji la mwanasoka bora wa Afrika na mchezaji wa
pekee wa Afrika kuwahi kushinda taji la Ballon d'Or mwaka 1995.
Alijipatia umaarufu katika klabu ya Monaco
1988 na kufanikiwa kuzichezea PSG na AC Milan muongo uliofuata.
Pia aliichezea Chelsea na Manchester City
katika ligi ya Uingereza katika miaka ya mwisho ya soka yake.
0 Comments