BEKI wa Liverpool, Virgil
Van Dijk amezidi kuonyesha ubora wake baada ya jana kupachika mabao mawili
wakati timu yake ya Liverpool ikishinda mabao 2-1 mbele ya Brighton.
Wachambuzi wa masuala ya
soka wanasema kuwa rekodi ya Liverpool kwa kasi yao washindwe wenyewe tu
kufikia malengo yao.
Mchezo huo wa Ligi Kuu
England ulikuwa na ushindani na ulishuhudiwa mlinda mlango wao namba moja
Allison Becker akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 76.
Mabao ya Dijk yalipatikana
yote kipindi cha kwanza dakika ya 18 na 24 huku lile la Brighton likipachikwa
dakika ya 79 ya kipindi cha pili na Lewis Dunk.
Ushindi huo unaifanya
Liverpool ibaki kileleni ikiwa na pointi zake 40 baada ya kucheza mechi 14 huku
nafasi ya pili ikiwa kwa mabingwa watetezi Manchester City wenye pointi 29.
0 Comments