Waziri mkuu Mstaafu na Mgombea wa Urais 2015
kupitia CHADEMA, Edward Lowassa leo alikamatwa na jeshi la Polisi wakati
akiwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome na baadaye
aliachiwa huru ambapo taarifa za polisi zinadai kuwa walimzuia kwa sababu
za kiusalama.
Kupitia kituo cha Television cha Azam
wameripoti habari ya kukamtwa kwa Lowassa ambapo baadhi wa wananchi wameeleza
ilivyokuwa.
"Tulikuwa kwenye msafara ya kumpokea Lowassa lakini
tulipofika hapa stendi wananchi walitaka kuongea na Lowassa, kabla hata hajashuka
kwenye gari askari walituvamia wakasema tuondoke moja kwa moja twende
kituoni"- shuhuda
0 Comments