DODOMA
Wakati mashirika ya umma 40
nchini yanayojiendesha kibiashara yakishindwa kutoa gawio kwa Serikali, Msajili
wa Hazina, Athuman Mbutuka amewataka wenyeviti na watendaji wakuu wa mashirika
hayo kujitathimini kama wanafaa kuendelea kuongoza mashirika hayo.
Mbutuka ameyasema hayo leo Novemba
24, 2019 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango kutoka
katika taasisi, mashirika na kampuni ambazo Serikali ya Tanzania ina hisa.
Amesema kati ya mashirika 81
yanayojiendesha kibiashara, mashirika 40 yameshindwa kutoa gawio kwa sababu
yanajiendesha kwa hasara.
Amesema anataoa rai kwa
wenyeviti na watendaji wa mashirika hayo wajitathmini kama wanatosha kuongoza
mashirika hayo huku akiyataka mashirika ya huduma nayo kupunguza utegemezi kwa
Serikali.
Msajili huyo amesema kiwango
cha makusanyo ya gawio kwa serikali kimeongezeka kutoka Sh bilioni 161.04 mwaka
wa fedha wa 2014/15 mpaka kufikia Sh1.05 trilioni mwaka 2018/19 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 552.
Mbutuka amesema ofisi yake imefanya
uhakiki wa mali zinazomilikiwa na Serikali na kubaini kuwa kuna nyumba 337,
viwanja 140, mashamba makubwa 10 na kampuni mbili ambapo amesema mali hizo zote
zimerudishwa serikalini.
Amesema wamebaini kuna kampuni
mbili ambazo hazipo kwenye orodha ikiwemo
kampuni ya Songwe Water Company ambayo Serikali inamiliki kwa asilimia
100 na kampuni ya Liquid Storage ambayo Serikali ina hisa ailimia 40.
0 Comments