SINGIDA -(picha kutoka maktaba )
Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya
Singida wametakiwa kufanya maandalizi ya kilimo mapema ilikuweza kuzitumia mvua
za kwanza katika shughuli hizo za kilimo.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Singida Bw, Elia Digha wakati akizungumza na standard
raedio kuhusu suala la maandalizi ya msimu ya kilimo.
Digha amesema wananchi wanapaswa
kuutumia vyema usemi wa mvua za kwanza ni zakupandia kwa kupanda mazao
mbalimbali ya chakula pamoja na biashara.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa
halmashauri ya wialaya Bw, Elia Didga amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza
chakula hususani katika msimu huu ambapo mazaokama mahidi yamepanda bei.
0 Comments