Katibu tawala mkoa wa Singida Dr Angelina Lutambi akitoa taarifa ya maendelea ya mkoa wa Singida baada ya waziri Hussein Mwinyi kuwasiri katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida. |
Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Martin Busungu akisikiliza taarifa hiyo kwa umakini. |
Mkurugenzi mtendaji wa Suma JKT Kanali Rajabu Mabele akimpamaelezo waziri Hussein Mwinyi wakati wa ukanguzi wa ukarabati wa jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa linalokarabatiwa na Suma JKT mjini Singida. |
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dakta Hussein Mwinyi amewagiza watendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa - SUMA JKT - kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotelezwa na shirika hilo kwa viwango vinavyotakiwa ili yaweze kutumika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi kwa muda muafaka.
Dakta MWINYI ametoa kauli hiyo mjini SINGIDA
wakati akikagua miradi inayotekelezwa na SUMA JKT ikiwemo ukarabati wa ofisi ya
Mkuu wa mkoa wa SINGIDA, ujenzi wa nyumba ya mganga mkuu wa mkoa ,Ujenzi wa
Jengo la Kuhifadhi Maiti katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa na kuonyesha kuridhishwa
na utekelezaji wa miradi hiyo.
Kwa upande wake, Katibu
Tawala wa mkoa wa SINGIDA Dokta ANGELINA LUTAMBI amesema Serikali ya mkoa imeamua kulipatia Shirika la SUMA JKT zabuni
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutokana na kasi na ubora wa utekelezaji wa miradi
kulingana na thamani ya fedha inayotolewa na Serikali.
Shirika la SUMA JKT kwa
mkoa wa SINGIDA linatekeleza miradi 12 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya
Shilingi bilioni 2.5
0 Comments