Wazee wa mkoa wa Singida wakimsimika na kumuombea kheri katibu mkuu mteule jumuiya ya wazai taifa. |
Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi taifa Mh Elasto Sima wakiinama kwa dk 1 kumuombea Mohamed Dewji Mo baada ya kupatikana kabla ya kuanza kuhutubia. |
Viongozi
wa ngazi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi CCM wametakiwa kuhakikisha
wanasimamia maadili ndani na nje ya chama ilikuhakikisha chama hicho kinakuwa
na viongozi wanaofuata maadili.
Kauli
hiyo imetolewa na katibu mkuu jumuia ya wazazi taifa wa Chama cha mapinduzi CCM
Bw, Elasto Sima wakati akizungunzia suala la maadili ndani na nje ya Chama.
Sima
amesema kwa sasa ndani ya chama wameanza kuchukua hautu kwa haraka huku
akizungumzia uchaguzi unao endelea huko zanziba.
Bw,
Sima amesema chama hakitasita kuwachukuli hatua kali wale viongozi wote
watakaoenda kinyume na kanuni na taratibu za chama hicho.
Amesema
kuwa endapo viongozi ngazi ya chama watakuwa na maadili itasaidia kupata
viongozi wa serikali wenye maadili mema.
0 Comments