CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida,kimeungana na Watanzania wengine
kumpongeza na hadi kupatikana kwa
mfanyabishara maarufu nchini, Mohammed Gullam Dewji akiwa hai.
Pongezi
hizo zimetolewa na katibu mwenezi CCM
mkoa wa Singida bw,Ahemed Athumani
wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kuachiliwa huru kwa
Mohamed Dewji.
Amesema
kwa kiasi kikubwa mafanikio ya kumpata MO akiwa hai,yamechangiwa na vyombo vya
serikali ya CCM,na maombi ya Watanzania wengi ambao ni wapenda amani na
utulivu.
Akisisitiza,alisema
MO alipendwa kwa uchangiaji wake mkubwa katika sekta mbalimbali za
maendeleo.Pia akiwa MNEC,pamoja na kazi kubwa aliyoifanyia CCM mkoa,aliweza
kujenga ofisi za kata (CCM) 116.
Alisema
wakati umefika kwa Watanzania waliobahatika kuwa na hali nzuri kiuchumi,kuajiri
walinzi kwa ajili ya usalama wao na wa mali zao.
Kwaupande
wake katibu wa CCM mkoa wa Singida,Amina
Imbo,amesema hadi sasa MO bado ni mpiga kura (CCM) mkoani hapa, na bado
anasaidia ustawi wa chama tawala mkoa bila kinyongo.
0 Comments