Kulia ni Bw Urbanus .F.Melkiori na Bw Wim Bredewold kutoka Arusha Technical College wakitoa ufafanuzi juu ya namna wanavyo toa elimu kwa vijana juu ya Nishati Jadidifu. |
Washiriki kutoka mikoa mbalimbali wakifuatila kwa makini maelezo kutoka kwa wawezeshaji. |
Kushoto ni katibu mkuu mtendaji Muhandisi Methew Matimbwi akiwa na baadhi ya watendaji kutoka TAREA ukumbini FDCT Utemini Singida mjini. |
Muhandisi Neema Msemwa Afisa viwango kutoka TBS akionyesha namna ya utambuzi wa kifaa cha kuzalishia umeme wa mwanga Sola chenye kiwango bora. |
Katibu Mkuu wa TAREA,Mhandisi Methew Matimbwi ameyasema hayo
kwenye semina ya siku moja iliyofadhiliwa na Benki ya dunia na kufanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) mjini Singida
na kuwashirikisha wauzaji wa rejareja wa vifaa vya umemenuru pamoja na
wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya wanani cha mjini Singida wanaochukua kozi ya
umeme.
Aidha Mhandisi huyo hata hivyo amebainisha kuwa bado wanaendelea
kufundisha vijana kwenye maeneo yale ambayo wanaona kuna uhitaji mkubwa kuliko
mwingine ambapo amekiri pia kwamba mahitaji ni makubwa sana ukilinganisha na
mafundi waliopo.
Naye Afisa viwango wa shirika la Viwango Tanzania (TBS)
akizungumzia namna ya kuwasaidia walaji wa Mkoa wa Singida ili waweze kununua
biadha zilizo bora,Bi Neema Msemwa ameweka wazi kuwa wao kama TBS wameshaanza
kufanya ukaguzi kwenye masoko makubwa kwa Mkoa wa Dar-es-Salaam kuwa ni pamoja
na Kariakoo,Tandika,Ilala na walikagua vifaa vya sola,nguo za ndani za mitumba.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambaye pia ni
mwuzaji wa vifaa vya umemenuru katika duka la SAMUSHO,Bi Elizabeth Masawe
amesema kwamba idadi kubwa ya bidhaa mbovu zimezagaa jijini Dar-es-Salaam na
TBS haijafanya jitihada zozote za kuzifuatilia kwa karibu mpaka zinawafikia
walaji wa mikoani.
BENKI ya dunia imefadhili tamasha ya siku mbili la nishati
jadilifu lililotanguliwa na semina kwa wauzaji wa rejareja wa vifaa vya
umemenuru pamoja na wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya wananchi wanaochukua
kozi ya umeme.
0 Comments