CCM MKOA WA SINGIDA YATOA TAMKO JUU YA MO DEWJI

Katibu mkuu wa ccm mkoa wa Singida Bi Amina Imbo.
SINGIDA
Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida,kimelaani kitendo cha kutekwa kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji.

Aidha,kimesema kitaendelea kumwombea kwa Mwenyezi Mungu ili aweze kupatikana akiwa hai.
Kimeiomba serikali na vyombo vyake,ifanikiwe kumpata MO  akiwa hai na wabaya wake wakamatwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Katibu wa CCM mkoa wa Singida,Amina Imbo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la kutekwa kwa Mohammed  
Katibu wa BAKWATA mkoa Singida Burhani Mlau,amesema BAKWATA inalaani kitendo cha kutekwa kwa mfanyabiashara huyo.

Amesema enzi akiwa mbunge,walishirikiana nae kwa karibu katika masuala ya dini na yale ya kijamii na hakuwa na chembe chembe ya ubaguzi wa aiana yo yote.
Naye Askofu mtaafu wa (FPCT) mjini kati,Paulo Samwel,amesema kanisa linaungana na watanzania wote wapenda amani, kukemea vikali kitendo alichofanyiwa Dewji.


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments