Mwanza
Amesema, nahodha huyo Abel Constatine ambaye pia alifariki
katika ajali hiyo, alikuwa mhitimu na alikuwa amefanya shughuli hiyo kwa zaidi
ya miaka 10.
Kuhusu kupakia abiria na mizigo kupita kiasi, amesema hilo
hawezi kulijibu kwa kuwa wakati wote wa shughuli ya upakiaji kazi yake inakuwa
kuangalia na kurekebisha mitambo na kuhakikisha chombo kipo imara kwa ajili ya
kuanza safari
Amesema licha ya kwamba kuna baadhi ya wenzake bado wapo
chini ya ulinzi kwa ajili ya mahojiano ameishukuru Serikali kwa kumruhusu
kwenda nyumbani kwake
Mhandisi huyo mkazi wa Kigongo Ferry, wilayani Misungwi
amesema hana sababu maalum ya kuikacha kazi ya uhandisi majini akitolea mfano
mafundi wa magari kwamba wakati gari linapopata ajali, mafundi na madereva
wanaendelea na kazi kama kawaida.
Kuhusu kukaa majini kwa zaidi ya saa 48, amesema ni miujiza
ya Mungu na kushukuru kwamba wakati kivuko hicho kinapinduka, alikuwa kwenye
ofisi yake akiendelea na shughuli kama kawaida.
0 Comments