|
Piki piki 28 zimetolewa na serikali wilayani Ikungi kwa lengo la kuinua Elimu kuanzia ngazi ya kata nchini |
|
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ikungi Bw Solomoni Kasaba akiongea wakati wa hafla fupi ya kukabidi pikipiki hizo. |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi na Diwani Mh Juma Ali Mwangi akimkaribisha mgeni rasimi Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu. |
|
Mgeni Rasimi Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu. |
|
Ikumbukwe kuwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzani Dr John Pombe Magufuli hivi karibu wakati akiongea na watanzania mkoani Singida alitoa wito kwa wakuu wa wilayanchi kuwa wakati wa kukabidhi pikipiki hizo ni lazia warati hao wasaini mkataba ili kuepuka ubadhilifu hapo mmoja wa waratibu akisaini mkataba huo. |
|
Mkuu wa wilaya wa Ikungi Akitesti pikipiki hizo na Mkurugenzi wa Wilaya ya Ikungi Justice Lawlance Kijazi. |
|
Afisa usalama barabara Polisi wilaya Ikungi akitoa maelezo juu ya matumizi ya barabara. |
Halmashauri ya wilaya ya IKUNGI mkoani SINGIDA imetekeleza
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI lililotaka
viongozi wa wilaya na mikoa kugawa haraka pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa
ajili ya Maafisa Elimu wa kata kama hatua ya kusaidia maafisa hao kutekeleza
majukumu yao ya kuboresha elimu katika maeneo yao.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pikipiki 28 zenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80
kwa maafisa elimu wa kata, Mkuu wa wilaya ya IKUNGI MIRAJI MTATURU
amewataka maafisa hao kuzitunza vizuri pikipiki hizo na hatasita kuchukua hatua
kwa maafisa elimu hao ambao watatua pikipiki katika shughuli zao binafsi.
Mtaturu amesema kilichobaki ni kuja kufanya tathimini baada
ya kuwakabidhi maafisa hao pikipki.
Tuandikie Maoni Yako Hapa
0 Comments