MARUFUKU KUINGIA NA KUCHA NA KOPE BANDIA BUNGENI, JE? WAGENI WAALIKWA


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amepiga marufuku wabunge kuingia bungeni wakiwa na kucha na kope bandia.
Akitoa maamuzi yake Bungeni leo asubuhi, Spika Ndugai amesema ataendelea kupokea maoni kuhusu suala la wabunge kuchibua ngozi zao.

Spika Ndugai amesema marufuku hiyo pia itawahusu raia ambao watakaokuwa wanatembelea Bunge hilo ambalo lipo jijini Dodoma.
Ndugai ametoa maamuzi hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalaum Bi Fatma Toufiq kuiuliza serikali juu ya athari za kiafya za matumizi ya kucha na kope bandia pamoja na uchubuaji wa ngozi.
Naibu Waziri wa Afya wa Tanzania Dk. Faustine Ndugulile alilieleza Bunge kuwa matumizi ya urembo huo bandia yanaathari kubwa kwa binadamu na kutaka jamii iepukane nayo.


Kwamujibu wa Ndugulile, kwa mwaka mmoja, takribani wagonjwa 700 hupokelewa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yatokanayo na kijichubua.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments