|
Mwnyekiti wa uchaguzi Bw Festo Sanga akitoa maelekezo kwa wapiga kura kushoto ni katibu wa kamati ya uchaguzi Mzee Damian Mkumbo kutoka gazeti la Majira Singida . |
|
Elisante Mkumbo wa ITV akiuliza swali meza kuu haipo pichani. |
|
Elisante John wa ETV Singida akitaka ufafanuzi wa jambo flani kutoka meza kuu. |
|
wagombea nafasi ya ujumbe wa kamati tendaji Bw Bonnface Jiriri na Shaban Msangi wakijinadi. |
|
Msimamizi wa uchaguzi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Bw Peter kashinje akionyesha kisanduku cha kupigia kura. |
|
Mwenyekiti mteule wa Singpress kulia Bw Seif Takaza akipongezwa na Festo Sanga (Suti nyeusi) mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi baada ya uchaguzi kumalizika na kumpisha katika nafasi yake. |
|
Emmanuel Michael wa Star tv makamu mwenyekiti mteule kushoto na Shabani Msangi afisa habari wa jeshi la polisi aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa Singpress wakipongezana baada ya uchaguzi. |
|
Mkurugenzi mtendaji wa umoja wa vyama vya waandishi wa Habari nchini UTPC Bw Abubakar Karsan akitoa salama za UTPC kabla ya uchaguzi kuanza. |
|
Bw Self Takaza mwenyekiti mteule akiongea baada ya kuchaguliwa . |
|
Kamati ya utendaji ya Singpress ikipozi kwa picha baada ya uchaguzi huo. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari (UTPC) Bw Abubakar Karsan akitangaza matokeo ya uchaguzi. |
Mkutano mkuu wa dharura
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Singida,umemchagua Seif Takaza kuwa
mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
Takaza amenyakua
nafasi hiyo baada ya kupata kura
10,akifuatiwa na Shaban Msangi,aliyepata
kura tano,na mgombea mwingine Elisante John kura mbili.
Akitangaza matokea
mengine,mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari (UTPC)
Tanzania,Abubakar Karsan,amesema mgombea pekee wa nafasi ya makamu
mwenyekiti,Emmanuel Michael,amepata kura zote 18 zilizopingwa, sawa na aslimia
mia moja.
Aidha Bw Karsan
limtangaza Revocatus Phinias kuwa katibu mtendaji baada ya kupata kura tisa
akifuatiwa na Abby Nkungu aliyepata kura saba, na Ramadhani Ngoi,aliyepata kura
mbili.Nafasi ya katibu msaidizi,imechukuliwa na Shaban Msangi.
Aidha,Karsan amesema
Teddy Mande mgombea pekee wa nafasi ya mweka hazina,amerejea kwenye nafasi yake
hiyo,baada ya kupata kura 18 zilizopingwa. Huku Respicius Cares Katemana,pia
amerejea katika nafasi yake ya mweka hazi msaidizi,baada ya kupata kura 17 za
ndiyo.
Katika hatua
nyingine,Karsan amewataka wanachama wa Singpess kushirikiana na uongozi wao
mpya,ili kuharakisha kuiletea maendeleo klabu yao.
Kwa
upande wake mwenyekiti mteule,Takaza,pamoja na kuwashukru wapinga kura,ameomba
ushirikiano wa karibu na wanachama na viongozi waliochini yake,ili kuipaisha
klabu hiyo kimaendeleo.
Tuandikie Maoni Yako Hapa
0 Comments