So sorry nilisahau ku
attach picha na bahati mbaya nikawa offline muda mwingi, kama zinaweza kutumika
kwa sasa picha hizi hapa ila kama muda utakuwa umekwisha basi hakuna namna
asante sana kwa ushirikiano wako.
Wakulima wakipata
maelezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo wa halmashauri ya Wilaya ya Momba katika
banda la maonyesho ya nanenane, juu ya njia rahisi ya kupanda mboga za majani
kwa kutumia magunia na mifuko hususan mahali pasipo na maeneo ya kupanda
bustani.
Mhifadhi wa Mazingira na kilimo hai kutoka
Wilaya ya Songwe Noah Ambokile Mbilinyi akitoa maelezo kwa Eddie Mhelela kuhusu
aina mpya ya maboga ambayo yana uzito wa Kilogramu 15 mpaka 25 katika banda la
wilaya ya Songwe kwenye maonyesho ya nanenane.
Wanafunzi wakijifunza kutoka kwa Afisa
Kilimo Sosten Lipamila kuhusu kilimo cha viazi sukari (beetroots) katika banda
la halmashauri ya Tunduma, beetroots zina madini mengi ya Calcium hivyo
hutumiwa kwa juisi, mboga na chakula na husaidia kuongeza damu.
Mwanzilishi wa kikundi cha kutunza Mazingira
cha Estate Vision Amani Zakaria Elias akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi
waliojitokeza katika banda la maonyesho ya Nanenane katika halmashauri ya
Wilaya ya Ileje, kikundi hicho kimeonyesha upekee kwa kuweka miche ya miti ya
mtini na mizeituni ambayo ni adimu kupatikana.
Afisa Kilimo kutoka shirika la Norwegian
Christian Aid Daniel Isaack akitoa maelezo katika maonyesho ya nanenane
kuhusu teknolojia rahisi ya umwagiliaji wa matone ambayo inaweza kutumia maji
lita 20 kumwagilia miche 52 ya mbogamboga, wakulima takriban 50 wa wilaya ya
Mbozi wameanza kutumia teknolojia hii.
0 Comments