JESHI LA POLISI SINGIDA LA MSHIKILIA MKAZI MMOJA KWA UBAKAJI

Kamanda wa Mkoa wa Singida ACP Sweetbert Njewike

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mkazi wa kijiji cha Mgundu Wilayani Iramba kwa tuhuma za kumlawiti Mwanafunzi wa kiume hadi kufa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Nalogwa John ambaye alimlawiti Mwanafunzi wa Darasa la Nne mwenye umri wa miaka 12
Amesema Agosti 25 mwaka huu majira ya saa 11.30 jioni wakati marehemu akiwa na mdogo wake wakichunga mifugo, mtuhumiwa alijitokeza ghafla na kumkaba shingo marehemu na kisha kuanza kumlawiti mbele ya mdogo wake.

Amesema baada ya mdogo wake kuona hivyo, alikimbilia nyumbani na kwenda kutoa taarifa kwa mama yao ambapo mama naye alitoka mbio hadi kwenye tukio lakini alimkuta mwanae amepoteza maisha huku mtuhumiwa akiwa bado ameduwaa
Amsema kuwa baada ya mama kupiga kelele ya kuomba msaada, wananchi walikuja haraka na ndipo mtuhumiwa alipozinduka na kukimbilia nyumba za jirani ili kujificha lakini walifanikiwa kumkamata.



Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments