Mesut Ozil amejiondoa kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani
akisema amestaafu kwa sababu ya UBAGUZI WA RANGI na DHARAU kutoka kwa Chama cha
Soka Ujerumani (DFB) na mashabiki.
Ozil mwenye asili ya Uturuki amekuwa akituhumiwa kuonyesha
kiwango duni wakati wa Kombe la Dunia nchini Urusi ambako Ujerumani ilivuliwa
ubingwa.
Hadi anatangaza kustaafu soka la kimataifa, Ozil ameichezea
Ujerumani mechi 92, amefunga mabao 23.
Aliisaidia kubeba Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Mwaka
2012 walifika nusu fainali ya Euro na 2016 wakabeba ubingwa.
Alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 2009 na
2010 alikuwa katika kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia kama 2018.
0 Comments