ALICHOKISEMA JERRY KUHUSU YANGA



Kuna taarifa kuwa Leo Unafanya Mkutano na Waandishi wa Habari, kama ni kweli Soma Haya kwanza kisha Uende na Kama sio, basi soma pia ujiandae kwa Mkutano najua lazima utakuwepo mkutano Aidha wa Vyombo vya Habari au Mkutano na Wanachama .

Pole na unapopitia, wewe ni Kaka yangu na Rafiki Yangu lazima nikwambie ukweli Japo utaumia ila utakusaidia.


1. Kama ulikuwa Unawaza kujiuzulu , Anza kwanza kumwajibisha Hussein Nyika, Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili.


Huyu amekuwa Chanzo cha Anguko lako, kama ulishindwa kumshauri au kama yeye alishindwa kukushauri basi Naomba ujue Wanachama Wengi sana Wameshajua Uchafu na Ufedhuli wa huyu mtu, ukipita mitaani na vijiweni utayasikia Haya.


Anatajwa kuiba fedha zinazochangwa na wajumbe wa kamati ya Mashindano na fedha hazipelekwi kunakohusika kama unabisha Muulize Mkwasa atakwambia hata kama Kaondoka.


Anasajili Wachezaji Dhaifu kwa kuwa tu anaweka cha Juu, kama unabisha ita Wachezaji kisha wape vikaratasi waandike pasipo kuweka majina yao utaona Ukweli wa hili, ushahidi Upo baadhi ya Wachezaji wamesema na wako tayari kusema, ila hawana Imani na nyinyi mana ni wale wale tu.


Kwanini awe mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na wakati huo huo awe mwenyekiti wa kamati ya usajili? Unajua kwa nini? Ngoja nikwambie anatunza mtandao wa 'Kuiba' hela mana mzunguko wote anao yeye, pia hivi Yanga hakuna mtu wa kusaidia kamati moja hapo? Why yeye tu? Huyo ni Kisalu au chambo wa Wizi nyuma yake wako Mapapa.


2. Sanga kabla hujazungumza Hebu toa ufafanuzi wa Fedha za Sports pesa milioni 240, pia toa taarifa ya Fedha za CAF zaidi ya milioni 200 , najua utasema Mlilipa madeni, kama ndivyo basi jibu na hili madeni Gani wakati Wachezaji wanadai mishahara ya Miezi 3 inakuwaje.


Najua utasema ulilipa madeni ya zamani, Sanga madeni gani hayo wakati uko zamani mlikuwa mnapata hela za Vodacom, Hela za Azam kupitia ufadhili na pia Yanga TV hapa mnapata hela nyingi tu, Vipi kuhusu hela za Udhamini wa Maji Afya? Hivi hizi hela mlikuwa mnazifanyia nini zamani mpaka mchukue milioni 440 mkalipe madeni ambayo baadhi ni madeni Hewa!!!


3. Sanga Naomba utuambie wewe kama Makamu mwenyekiti wa Yanga ulifanya nini katika Kumshauri Mwenyekiti wako  wakati anapandidha Gharama za Uendeshaji wa Klabu bila kuwa na vyanzo Halali vya fedha vya Yanga? Kwanini ulikaa kimya Ukafumbia Macho jambo hili ambalo Leo limekuwa sababu kuu ya Kuitesa Yanga?


Mwenyekiti kapandisha gharama za uendeshaji wa klabu bila kushauriana na mtu au kikao au wanachama wewe kama makamu umekaa kimya Hii ni DHAMBI kubwa sana ulifanya na sasa INAKUHUKUMU.


Laiti Ungejua kuwa Hicho ni KITANZI chako ambacho Leo ndio kinakunyonga MWENYEWE , kwa kuwa Hukuwa Na akili, na maarifa na Ubunifu wa kutosha Ukakaa kimya na kuchekelea fedha Za ' MUHINDI ' leo amekugeuka Unajuta, mana kapandisha gharama za uendeshaji kwa kusajili Wachezaji kwa gharama za juu sana,mishahara minono kisha akakususia pasipo kukupa hela za kuendesha klabu Leo KAMUSOKO , SHISHIMBI na wengine wanaanza kufunga virago, Pole sana kaka yangu.


4. Kujiuzulu kwa MKWASA , nilitegemea ungejifunza kwake Pamoja na Mapungufu yake MKWASA alipaswa kuwa Mshauri wa benchi la Ufundi au Kocha wa Muda wa Yanga, badala yake mkaendelea Kumpuuza na kumtesa, Hela wapige wengine, Lawama kwa Mkwasa tu, Mwache apumzike kwa sasa Huenda Akarudi Yanga kama Kocha au mshauri wa Benchi la Ufundi wakati Ukifika. 


HITIMISHO 


Najua Clement Sanga kwa sasa hauko Vizuri kiuchumi , na wewe una Majanga yako unayopambana nayo, Nakushauri kabla Hujazungumza kitu TUBU na omba RADHI kwa kusema ukweli, usijaribu kutoa sababu japo zipo sababu za Kawaida sana, ila sababu hizo Hapo juu ndio ZIMEKUMALIZA .


Ukishamaliza Haya, basi omba kujiuzulu, halafu Kaa kimya Endelea na Maisha yako, itakusaidia uko Mbele, usijaribu KUMTWISHA mtu Mzigo wako.


Tunaitaka Yanga ile ya Kimataifa.


 Ngariba Mkuum Jerry Murro

 MwanaJangwani
 23/07/2018

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments