Mkuuwa wilaya ya Iramba akifika katika Hospitali ya wilaya ya Iramba. |
dereva wa lori la Azam Bw,Nelsoni Sanya (38) akisimuli jinsi ajali hiyo ilivyotokea aliyesimama ni mkuu wa wilaya ya Iramba Emanuel Huhaula alipofika katika kituo cha afya kilichopo wilayani Iramba. |
WATU wawili wa familia moja wamepoteza maisha
kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu na kuligonga gari dogo aina ya HICE
lenye namba za usajili T149 DAF walilokuwa wakisafiria kutoka Mkoani Arusha
kwenda Kijiji cha Shelui wilayani Iramba,Mkoani Singida kugongwa na gari lenye
namba za usajili T791 CBW aina ya Benzi katika Kijiji cha Kizaga,barabara kuu
ya kutoka Singida kwenda Mwanza.
Mganga Msaidizi wa Hospitali ya wilaya ya
Iramba,Dk.Revocatus Akaro amethibitisha kupokea miili ya watu wawili
waliopoteza maisha na kuwataja kuwa ni Bwana Julius Kiula( 50),Bi Mwaridieli
Mdede (48) na dereva wa lori,Nelsoni Sanya (38) aliyekuwa majeruhi katika ajali
hiyo.
Kwa mujibu wa daktari huyo Kiula alikuwa na
jeraha kichwani lililochangia kifo chake na Mwaridieli Mdede alikuwa na jeraha
kichwani na mbavu za upande wa kushoto na wa kulia wakati dereva wa lori ambaye
ni majeruhi,alikatwa sehemu ya kanyagio la mguu wa kushoto na kushonwa nyuzi
tisa na hali yake inaendelea vizuri.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye
pia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba,Bwana Emmanueli Luhahula amesema tukio hilo
lilitokea julai,21,mwaka huu saa tano asubuhi ambapo polisi wa kitengo cha
usalama barabarani walisimamisha gari dogo aina ya Hice na lori yaliyokuwa
yakienda mwendo wa kasi na kuanza kuwahoji wahusika.
Ameweka bayana Luhahula kwamba wakati
mahojiano yakiendelea ndipo ghafla lilitokea lori la Kampuni ya Azamu na wakati
likitaka kupita ndipo askari walijitokeza na kulisimamisha ghafla na ndipo
dereva alipotaka kufunga breki,tairi la mbele lilipasuka na gari likayumba na
ndipo tela lake lilipoigonga hice iliyokuwa na watu wawili wa familia moja.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya huyo amekiri kwamba
jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kilifanya makosa kwa kusimamisha
gari kwa pande zote mbili na kila upande kukawa na gari na kuifanya barabara
hiyo kubakia kuwa ndogo na pia kukimbilia kusimamisha gari ghafla,lililokuwa
likienda mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo kutokea.
Akizungumza huku akiangua kilio kwa uchungu wa
kupoteza ndugu zake wawili,dereva wa gari dogo aina ya Hice,Bwana Gunda Mdede
amesema akiwa safarini kutoka Arusha kwenda Shelui ndipo alipofika kwenye eneo
hilo,askari wa kikosi cha usalama barabarani walisimamisha ghafla gari pande
zote za barabara.
0 Comments