Mh Mussa sima mbunge wa jimbo la Singida mjini akisikiliza matatizo ya wananchi katika kata ya Njuki pembeni yake ni diwani wa kata ya mandewa Mh Bakari Ntandu
|
Katika jitihada za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli za kuhakikisha elimu inatolewa bila malipo.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mussa Ramadhan Siima ameunga mkono
kwa kuhakikisha anajenga shule mbili za kidato cha tano na sita Singida mjini
ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Pombe Magufuli za
kuhakikisha elimu inatolewa bila malipo .
Sima amebainisha hilo wakati akizungumza na Standard Radio ambapo
amesema mkoa wa Singida hauna shule ya hadhi hiyo achilia mbali shule ya Mwenge ambayo ni ya kitaifa ambapo
shule moja wapo kati ya hizo itakuwa imekamilika kabla ya uteuzi wa kidato cha
tano kumaliza miezi miwili ijayo.
Ameishukuru Serikali ya awamu ya 5 kwa kutoa kipaumbele katika
suala la Elimu kwa kuhakikisha mazingira ya utolewaji wake yanaendana na lengo
kusudiwa.
Mh diwani wa kata ya Mandewa Bakari Ntandu akimkaribisha mbunge wa Singida mjini Mh Mussa Sima |
wananchi akiuliza swali kwa mbunge |
0 Comments