Afisa mipango wa TACAIDS Tanzania Bw Renatus Kihonga akifungua mkutano huo. |
Mkutano wa kazi waTume ya
kudhibiti ukimwi Nchini Tanzani (TACAIDS) umeanza mkoani Singida ukikutanisha
mikoa kumi na halmashauri thelathini wenye lengo la kufanya tadhimin ya
matumizi ya fedha zinazotolewa kwaajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI.
Akiongea katika mkutano huo wa
siku mbili ulioanza jana katika ukumbi wa chuo cha ufundi stadi VETA afisa
mipango wa TACAIDS Tanzania Bw Renatus Kihonga amesema mbali na kufanya
tahimini wanaajenda ya kutafuta rasilimali za ukimwi ambapo kwasasa wafadhili
wameanza kupungua.
Amesema wao kama tume ya
kudhibiti ukimwi nchini wameweka mikakati mbalimbali ya kutafuta rasilimali
ilikuweza kupambana na uhaba wa wadhamini katika mapambano ya UKIMWI
Bw,Kihongo amezipongeza secta
binafsi kwa mchango wao katika kupambana dhini ya UKIMWI .
Kwa upande wa mkurugenzi wa
fedha na utawala wa TACAIDS Bw Yasin Bassi amesema wadau wa ndani ya nchi bado
wanayo frusa kubwa ya kutoa mchango wao katika mapambano hayo.
0 Comments