Maandamano yakiingia katika uzinduzi wa wiki ya elimu duniani inayoratibiwa na mtandao wa Elimu nchini Ten Met. |
Mkuu wa mkoa Dr Nchimbi akisakata Rumba na wanafunzi kutoka mashule mbali mbali baada ya kupokea maadamano. |
Bi Cathline Sekwao Mratibu kutoka Mtandao wa Elimu Nchini Ten Ment akisoma Risara mbele ya mgeni rasimi Dr Rehema Nchimbi wakati wa uzinduzi wa Juma la Elimu kitaifa wilayani Mkalama Mkoani Singida. |
Mkoa wa Singida umeongeza idadi ya uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza
kutoka elfu arobain na tatu na mianane
arobaini na kufikia elfu sitini na nane miatisa themanini na tisa ikiwa ni
jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika secta hiyo ya elimu.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa juma la elimu ambalo lilizinduliwa May 14 wilayani Mkalama
Singida mkuu wa mkoa Dr Rehema Nchimbi amesema hiyo ni mikakati na jitihada
mbalimbali na serikali katika kuweka mkazo juu ya elimu nchini.
Amesema
ongezeko hilo linatokana na mkakati wa elimu bure suala ambalo linalenga kutoa
haki sawa kwa wote kupata elimu.
Dr,
Chimbi ameutaka mtandao wa elimu nchini Tanzania TEN MET kutekeleza
miradi yao inayohusu elimu kwani serikali ya awamu ya tano nayo imejipambanua
Zaidi kuwekeza katika elimu.
Kwaupande wake Bi,Cathelin Sekwao ambaye ni Mratibu
mtandao wa elimu tanzani amesema lengo la kuweka juma la elimu ni kuhamasishana kushirikiana ilikuweza
kutetea haki ya mtoto ya kupata elimu.
0 Comments