Na,Jumbe Ismailly MANYONI
WAKULIMA wa zao la tumbaku wa Chama kikuu cha wakulima wa
tumbaku (CETCU) Kanda ya kati wameamua kubadili kilimo cha zao la tumbaku na
kuingia kwenye kilimo cha mazao mchanganyiko kama vile pamba,korosho na alzeti
baada ya makampuni yanayonunua tumbaku kubadilisha masharti ya upatikanaji wa mikopo
wanayotoa.
Akisoma taarifa kwenye mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi kwa
niaba ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake,Bwanad Florence Mpana,katibu wa chama
cha msingi Msemembo Amcos,Bwana Laurenti Mwang’imba amesema kutokana na hali ya
kilimo cha tumbaku kuwa na vikwazo vingi,hivyo wamelazimika kubuni mradi wa
kilimo cha mazao mchanganyiko.
Aidha Bwana Mpanda amefafanua kuwa mradi huo utasimamiwa
na union ili mwisho wa siku union iwe na chanzo chake cha mapato
yatakayosaidiana na ushuru unaotokana na mapato yanayopatikana kutoka kwenye
Amcos.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo aliyemaliza muda wake,Cetcu
inahitaji shilingi 80,000/= kwa ajili ya shughuli za usafishaji kwa
kutumia greda ambalo linafanyakazi kwa usimamiza wa uongozi wa Halmashauri ya
wilaya ya Manyoni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CETCU Kanda ya kati,Bwana Daudi
Ngayaula amesisitiza kwamba kutokuwepo kwa mazingira rafiki kati ya Chama
Kikuu cha Wakulima wa tumbaku Kanda ya kati (CETCU) Mkoa wa Manyoni,Wawekezaji
pamoja na Taasisi za kifedha kulichangia chama hicho kukimbiwa na wanunuzi wa
zao hilo na hivyo kusababisha wakulima kushindwa kulipa madeni yao wanayodaiwa
na taasisi hizo za kifedha.
Aidha Bwana Ngayaula ameweka bayana kwamba endapo wawe ekezaji
hao watakuwa na imani watawekeza Manyoni kwenye biashara ya tumbaku na hatimaye
mwisho wa siku fedha zao watapata na wakulima watapata faida.
Kwa upande wake Meneja wa CETCU Kanda ya kati,Bwana Simon Hoja
amewataka wakulima wa zao la tumbaku kuhakikisha wanapanda kwanza miti na
kujenga mabani ya kisasa kabla ya kuanza kilimo cha zao la tumbaku.
Akifungua mkutano huo maalumu,Katibu tawala wa wilaya ya
Manyoni,Bi Rahabu Mwagisa ameweka bayana kwamba kati ya vyama vya ushirika vya
msingi vya tumbaku 21 vilivyokuwepo,lakini kutokana kutokana na
changamoto mbali mbali za uongozi,vyama 16 vimekosa usajili kufuatia
mzigo wa madeni ya muda mrefu ya zaidi ya shilingi bilioni 11.
0 Comments