CHAMA cha Netbali Tanzania (CHANETA) kimeanzisha Programu
maalumu ya kuhamasisha mchezo wa Netbali kuanzia ngazi ya wilaya,Mkoa hadi
Taifa ili kuhakikisha kiwango cha mchezo huo kinakua kwenye maeneo yote
nchini badala ya sasa ambapo mchezo huo kwenye baadhi ya mikoa umeanza kutoweka
kabisa.
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji CHANETA Taifa, YASINTA SILIVESTER
ameyasema hayo kwenye mafunzo ya walimu wa mchezo wa Netbali yaliyohudhuriwa na
walimu 19 wa shule za msingi na sekondari Mkoani Singida na kufanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenge mjini Singida.
AIDHA YASINTA amesisitiza pia kwamba mwezi wa nane, mwaka huu
kutakuwa na semina ngazi ya taifa,hivyo walimu waliohudhuria mafunzo hayo
yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari Mwenge,angependa wasinyimwe
ruhusa ya kuhudhuria mafunzo hayo yatakayofanyika Mkoani Manyara.
AKIZUNGUMZA na walimu wa michezo waliohudhuria mafunzo hayo ya
siku tano,Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,HENRY KAPERA pamoja na mambo
mengine ametumia fursa hiyo kuvipongeza vituo vya Televisheni vya CHANNEL
TEN na AZAMU kwa mchango wao mkubwa wa kutangaza michezo katika Mkoa huo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa
kwenye picha ya pamoja na mgeni rasimi Afisa michezo mkoa wa Singida Bw Henry
Kapela mwenye tsheti nyekundu wa tatumstali wa nyuma waliyo simama.
0 Comments