Balozi wa Ireland nchini Bw Poul Sherlock na ujumbe wake akizungumza na mkurugenzi na mmiliki wa kituo cha Radio Standard Fm Singida Bw James Daudi ofisini kwake |
Kamanda msaidi wa jeshi la polisi Bw Puge akiongea na watangazaji wa Standard radio nje ya ofisi . |
Mkurugenzi mkuu na mmiliki wa Standard Radio fm akifafanua jambo. |
Bi Bronagh Carry afisa mausiano wa ubalozi wa Ireland akifafanua jambo |
Picha ya pamoja na wafanyakazi baada ya kikao. |
Bw James Daudi akimwelezea juu ya ukarabati wa Studio mpya Balozi Poul Sherlock wa Ireland baada ya kutembelea na kujionea namna ya ukarabati huo unavyoendelea. |
Balozi wa
Ireland hapa nchini Paul Sherlock ametembelea standard radio na kufanya
mazungumzo na uongozi wa Standard radio.
Akwa standard Radio ameipongeza Standard kwa
kuwa na vipindi vinavyoelimisha jamii na kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa
umma
Pia ameshauri Standard radio kuweka msitizo
katika vipindi vya kuelimisha jamii hasa kuzungumzia biashara ya watoto wa kike
kwenda kufanya kazi katika mikoa mabalimbali nchini.
Kwa upande mwingine amezungumzia kuhusu haki za
watoto na wanawake hasa katika kukabiliana na tatizo la ukeketaji kwa wanawake
mkoani Singida
Naye Mkurugenzi wa Standard radio bw James
Dudi amemshukuru balozi huyo kwa kuona umhimu wa kuitembelea Standard
radio na kwa ruzuku ambazo zimekuwa zikitolewa na ubalozi wa Ireland kupitia
taasisi inayotoa ruzuku kwa vyombo vya habari tanzania (Tanzania media
Foundation).
Bw James
amesema kupitia ruzuku hizo Standard
Radio imeweza kujengewa uwezo wa kitalaam na vifaa mbalimbali.
Katika ziara hiyo balozi Paul Sherlock
ameambatana na msimamizi wa miradi ya maendeleo
pamoja na olive kinabo mshauri wa masuala ya jinsia.
0 Comments