PROF LIPUMBA SEKTA YA ELIMU NCHINI BADO NI CHANGAMOTO

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF) Prof Lipumba akiongea wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la singida kaskazini zinazoelekea ukingoni hivi karibuni.


Wasanii mbalimabli wakicheza na kuiba.

Na,Jumbe Ismailly SINGIDA  
CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa pamoja na serikali ya awamu ya tano kufuta ada katika shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini sekta ya elimu bado haijawekeza ipasavyo kwenye sekta hiyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kuikabili sekta hiyo mpaka sasa.

Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho,Bi Delphina  Mngazija uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini.Amefafanua kiongozi huyo wa kitaifa kwamba serikali inapowekeza kwenye sekta ya elimu kwa sasa ni lazima pia iwekeze kwenye matumizi ya kompyuta kwenye shule zilizopo na kuongeza kuwa elimu ya siku hizi inakwenda sambamba na mitandao ya kompyuta.

Kwa mujibu wa Prof.Lipumba nchi nyingi pamoja na nchi maskini zimewekeza mara tu watoto wanapoanza hujifunza pia kutumia kompyuta na kwamba matumizi ya kompyuta ni sawa kama vile kujifunza lugha.

Prof.Lipumba hata hivyo ametumia fursa hiyo kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa vituo vya afya vilivyopo kuwa na virutubisho muhimu na kwamba kutokana na taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha.

Naye Katibu wa CUF Mkoa wa Singida,Bwana Selemani Ntandu amewatahadharisha wanachama wa CUF pamoja na wale wa CCM waishio katika Kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla kwamba endapo watamchagua mgombea wa CCM,Bwana Justine Monko wakae wakijua kwamba makao makuu ya wilaya hiyo yatahamishwa kwenda Kijiji cha Sagarumba badala ya Ilongero.

Aidha katibu huyo amesisitiza kwamba wananchi wa jimbo la Singida kaskazini wanahitaji huduma bora za kijamii zilizoboreshwa na kuonyesha masikitiko yake kwamba hivi sasa miundombinu ya barabara kwenye maeneo mengi hairidhishi kabisa jambo ambalo halishughulikiwi na watu waliokabidhiwa dhamana ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho. 

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments