DR NCHIMBI AKAGUA KIWANDA CHA MOUNT MERU BAADA YA UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA MAJI.

Dr Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama  mkoa akiongea na uongozi wa kiwanda cha Mount Mreu mjini Singida mara baada ya kukagua kiwanda hicho.


Bw Nelson Mwakabuta afisa mausiano wa kiwanda hicho akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi. 




Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi, amesema hatarajii kuona kiwanda chochote katika mkoa wake kikifungwa, kwa kuwa maelekezo yote wanayo viongozi na watendaji wa serikali.
Ametoa kauli hiyo baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kutembelea kiwanda cha Mount Meru, ili kuona utekelezaji wa agizo la naibu waziri wa mazingira Bw Kangi Lugola, baada ya kufungwa kutokana na mapungufu kadhaa.
Amesema Elimu,taaluma, taarifa, maelekezo, sheria, mazingira ,sera ,na mazingatio yote viko mikononi mwa watalaamu,viongozi na watendaji wa serikali na kwamba wao kama watalaamu na watendaji ndio wenye dhamana ya kuvilea viwanda hivyo, na kuhakikisha vinaendeshwa na kufanya kazi kama inavyotakiwa.
Ameagiza watendaji na watumishi wa serikali ,kuhakikisha utalaam wao unakuwa sehemu ya uendeshaji wa viwanda hivyo ,kila siku.

Amesema viwanda vya singida vilivyopo kwa sasa, vikifanya vizuri vitavutia wawekezaji wengine kuwekeza katika mkoa wa Singida, ambao awali haikuwa na sifa ya uwekezaji ,wa viwanda.

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments