Meneja Uhusiano wa kiwanda cha Mount Meru Bw Nelson Mwakabuta |
Uongozi wa kiwanda cha Mount Meru
Millers Ltd tawi la Singida umeanza rasmi kutekeleza maagizo ya serikali na
umeahidi kukamilisha kazi hiyo mapema iwezekanavyo, ili wafanyakazi na wakulima
wa alizeti wasiathirike kwa kitendo cha kufungwa kwa kiwanda hicho.
Kiwanda hicho kinachodaiwa kuwa
kikubwa katika nchi za Afrika mashariki,juzi kilifungwa jana kwa muda usiojulikana na naibu waziri
nchi,muungano na mazingira,Kangi Lugola,baada ya kukikangua kwa zaidi ya saa
mbili.
Kutokana na ukaguzi huo,Lugola alijiridhisha kuwa
maagizo yaliyotolewa na mtangulizi wake Mpina zaidi ya mwaka moja uliopita,
yalikuwa hayajafanyiwa a kazi .
Maagizo hayo ni pamoja na kulipa shilingi
20 milioni ikiwa ni faini ya kutiririsha maji taka na yenye kemikali kwenye
makazi ya watu na mengine,kwenye ziwa Singidani lenye samaki na viumbe vingine
hai.Agizo jingine ni kununua mashine maalum ya kutibu maji taka yanayotoka
kiwandani.
Meneja uhusiano na utumishi wa kiwanda
hicho,Nelson Mwakambuta,amesema leo asubuhi wameanza rasmi kutekeleza kwa
umakini mkubwa maagizo yote yaliyotolewa na serikali,ikiwemo kuweka mifumo ya
maji taka kwa mijubu wa sheria ya mazingira.
0 Comments