WANAHABARI WAKUTANA NA SINGIDA BLACK STARS (MEDIA DAY)


                         Jonathan Soha akiongea na calestv katika dimba la Namfua Mjini Singida.



Meneja wa Singida Black Star Amisi Tambwe asema hayo ni maneno tu sisi ni kazi kazi tuko Vizuri sana.

Singida

29.03.202

Katika siku maalum ya habari inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wanahabari kutoka mikoa mbalimbali, wakiwemo wa Singida, wanapata fursa ya kuzungumza na wachezaji wa Singida Black Stars leo tarehe 29 Machi 2025.

Blogu yetu imepata nafasi ya kufanya mahojiano maalum na Jonathan Soha, ambaye ameweka wazi mtazamo wake kuhusu kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana. Soha amesema kuwa Ghana ina wachezaji wengi wa kimataifa, hivyo hana wasiwasi na kiwango chake kwa sasa.

Pamoja na kucheza Ligi Kuu ya NBC, Soha amesisitiza kuwa yupo tayari kuitumikia timu ya taifa iwapo atahitajika. Aidha, ameonesha kuvutiwa na kiungo wa Yanga SC, Azizi Ki, akisema angependa kucheza naye endapo nafasi hiyo itatokea.5


Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments