Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akiongwa na mkuu wa wiliya ya Singida Bw Elis Tarimo |
Mgomgea kiti cha ubunge jimbo la Singida kaskazini Bw Justen Monko akikabidhiwa Irani ya chama na naibu katibu mkuu wa CCM taifa |
wananchi wa kata ya Mtinko waki sikiliza namna chama cha mapinduzi CCM kilivyozindua kampeni hizo. |
wabunge wanaotoka mkoa wa Singida wakimpongeza mgombea kiti cha ubunge katika uzinduzi huo wa kampeni za kuwania kiti hicho cha ubunge jimbo la Singida Kaskazini. |
Kazi za zaidi ya wanachama 100 wa chama cha Demoklasia na maendelea CHADEMA kutoka wilaya ya Singida wamejiunga na CCM |
MWENYEKITI
wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi ametoa
tahadhari kwa watu wanaotarajia kujitokeza na kutaka kuingilia mikutano ya
kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini zinazoendelea kufanyika
kwa usalama,amani na utulivu na kutaka kuzivuruga,serikali mkoani hapa
haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria.
Dk.Nchimbi
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida ametoa tahadhari hiyo katika Kijiji cha
Mtinko,wilaya ya Singida vijijini alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio kwenye
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida kaskazini yaliyopatikana
kutokana na serikali ya CCM iliyopo madarakani.
Katika
uzinduzi huo uliofanyika katika Kijiji cha Mtinko,Mwenyekiti huyo wa kamati ya
ulinzi na usalama amesisitiza kwamba ili waweze kutambua kwamba utumishi wake
ametumwa na Chama cha Mapinduzi,na hiyvo ajitokeze mtu yeyote yule
atakayethubutu na kutaka kujaribu kuvuruga ratiba hizo za uchaguzi.
Hata
hivyo Dk.Nchimbi ametumia fursa hiyo pia kwa kuwafahamaisha wanachama pamoja na
wananchi kwa ujumla kwamba mikutano ya kampeni yote itakuwa salama ikiwa ni
pamoja na uchaguzi huo mdogo utakuwa salama kwani serikali ya mkoa imejipanga
kikamilifu kudhibiti yeyote yule atakayeonekana anataka kuchangia kutofanyika
kwa uchaguzi huo.
Hata
hivyo Dk.Nchimbi ameyataja baadhi ya mafanikio yaliyopo katika jimbo hilo la
Singida kaskazini kuwa ni pamoja na bomba na mafuta ambalo kwa Singida
kaskazini lina sifa ya pekee yake na kwamba litakuwa limenyanyuka juu kuliko
sehemu yeyote litakapopita.
Mkuu wa
wilaya ya Ikungi,Bwana Miraji Mtaturu akizungumza na wanachama wa CCM amesema
kuwa wanaamini wao kama watumishi wa serikali wataitekeleza vizuri ilani ya CCM
iwapo watampata mbunge wa Chama Cha Mapinduzi.
Naye Meneja wa kampeni za uchaguzi mdogo wa
jimbo la Singida kaskazini,Bwana Elia Digha akimnadi mgombea wa chama hicho ameweka
bayana kuwa Halmashauri hiyo ina vituo viwili vya afya kati ya 21 vinavyotakiwa
na kwamba kuna baadhi ya ujenzi wa vituo vya afya vilivyoanza kujengwa kwa
nguvu za wananchi.
Uchaguzi
mdogo wa jimbo la Singida kaskazini unaotarajiwa kufanyika jan,13,mwaka huu
unafuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo,Lazaro Nyalandu kutangaza kuachia wazi
jimbo hilo na kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo.
Vyama
vinavyoshiriki katika uchaguzi huo mdogo ni pamoja na CCM,CUF,AFP,CCK na TADEA huku
mgombea wa CHADEMA aliyechukua fomu kugombea nafasi hiyo akitangaza kujitoa
kuendelea kushiriki katika uchaguzi huo.
0 Comments