Iramba -Singida
Na Mwandishi Wetu
Mahakama ya
Wilaya ya Iramba imemhukumu kifungo cha maisha Barnaba Yohana Isaya (20), mkazi
wa Kijiji cha Nselembwe, Kata ya Sherui, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida,
baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka
minne, mkazi wa kijiji hicho.
Baada ya
kutenda kosa hilo, mtuhumiwa alikamatwa na Jeshi la Polisi Februari 5, 2024,
katika Kijiji cha Nselembwe na kufikishwa mahakamani Februari 12, 2025, kujibu
tuhuma dhidi yake.
Akitoa
hukumu hiyo Machi 6, 2025, Hakimu wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Simon Kayinga,
alieleza kuwa baada ya Mahakama kujiridhisha bila shaka na ushahidi wa
mashahidi, mshitakiwa alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa
kitendo hicho cha ukatili.
Mheshimiwa
Kayinga ameongeza kuwa adhabu hiyo iwe fundisho kwa yeyote mwenye tabia za
ukatili kama huo.
0 Comments