Singida
Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imefanya kikao na watoa huduma za usafiri
mkoani Singida, lengo likiwa ni kutoa elimu kuhusu huduma wanazotoa pamoja na
kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.
Akizungumza katika semina hiyo ya siku moja
iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Rafiki Hotel, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Sheria wa LATRA Taifa, Bi. Mwadawa Sultani, amesema mamlaka hiyo ina utaratibu
wa mara kwa mara kukutana na wadau wake ili kutoa elimu na kutatua changamoto
zinazowakabili kwa pamoja.
Mwadawa Sultani: "Tunafanya hivi katika mikoa
yote nchini ili kuhakikisha sheria na kanuni zinafuatwa. Ni muhimu kukutana na
wadau ili kujua kama kuna ufanisi katika matumizi ya sheria za utoaji huduma za
usafirishaji."
Kwa upande wake, Kaimu Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi
la Polisi, Miguta Kubilu, akifunga mafunzo hayo, amewataka madereva na wamiliki
wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanafuata sheria za barabarani ili kupunguza
ajali.
Miguta Kubilu: "Ni wajibu wa kila dereva na
mmiliki wa chombo cha usafiri kuhakikisha wanazingatia sheria za barabarani ili
kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu."
Aidha, washiriki wa semina hiyo wameiomba LATRA
kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wamiliki, mawakala, na watoa huduma za
usafirishaji ili kuboresha sekta hiyo.
Wanufaika wa Mafunzo: "Tunaomba LATRA
iendelee kutufundisha na kutufikia zaidi ili kuhakikisha sekta ya usafiri
inakuwa salama na yenye tija kwa wote."
0 Comments