Mkurugenzi wa Mgonto Foundatiom Kassim Mumbwa amesema kuwa Mgonto Foundatio ni Taasisi ya Kijamii.
Wanahabari kutoka Vyombo mbalimabli Mkoani Singida wakipata Futari iliyoandaliwa na Chief Mgonto Foundation
Singida,
09 Machi 2025
Taasisi ya Mgonto Foundation imeandaa hafla maalum ya futari kwa wanahabari wa Mkoa wa Singida, tukio lililofanyika katika Hoteli ya Rafiki. Hafla hiyo ililenga kuimarisha mshikamano kati ya wanahabari na wadau wa maendeleo, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida, Elisante John, ambaye aliwashukuru waandaaji kwa kutambua mchango wa wanahabari katika jamii. Alisisitiza kuwa ushirikiano kati ya vyombo vya habari na taasisi kama Mgonto Foundation ni muhimu kwa maendeleo ya mkoa huo.
Akizungumza Mkurugenzi wa Mgonto Foundation Kassim Mumbwa alieleza dhamira ya taasisi hiyo ya kuendelea kushirikiana na jamii, ikiwemo wanahabari, ili kuimarisha umoja na maendeleo ya Singida.
"Tunatambua mchango mkubwa wa
wanahabari katika kuhabarisha na kuelimisha jamii. Mgonto Foundation itaendelea
kuwa karibu nanyi na wadau wengine ili kuhakikisha tunaleta maendeleo ya
kweli," alisema Mkurugenzi huyo.
Wanahabari walioshiriki hafla hiyo
waliipongeza Mgonto Foundation kwa kuthamini mchango wao na kuahidi kuendelea
kushirikiana na taasisi hiyo katika kufanikisha maendeleo ya jamii.
Hafla hiyo ni moja kati ya jitihada za
Mgonto Foundation katika kujenga mshikamano wa kijamii, huku ikiendelea
kusaidia makundi mbalimbali katika mkoa wa Singida.
0 Comments