Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akitoa taarifa juu ya maandalizi ya Mei Mosi kitaifa yatakayofanyika katika viwanja CCM LITI Mjini Singida.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania Henry Nkunda.
Singida
Maandalizi ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Singida. Akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amewataka wananchi wa mkoa huu kuwa tayari kwa fursa mbalimbali, hususan za kibiashara, zitakazojitokeza katika tukio hilo la kihistoria.
Tayari vikao vya maandalizi vimeanza, huku shughuli mbalimbali zikitarajiwa kufanyika kuelekea Mei Mosi. Miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni utalii wa ndani, ambapo barabara ya Kuku Vestivo itafungwa kwa ajili ya maonyesho ya vyakula vya asili vinavyopatikana mkoani Singida. Baadhi ya vyakula hivyo ni kuku, mbuzi, kondoo, kanga, sungura, na ng’ombe, ambavyo vitapatikana bure kwa wananchi. Sambamba na hilo, kutakuwa na michezo mbalimbali kwa burudani ya wakazi wa Singida na wageni.
Kuhusu suala la usalama, Mkuu wa Mkoa, Bi. Dendego, amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha sherehe hizi zinafanyika kwa amani na utulivu. Ameongeza kuwa usalama umeendelea kuimarishwa, huku akitoa wito kwa wadau kushirikiana ili kuhakikisha tukio hili linafanikiwa.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamuhokya, amesema kuwa maandalizi ya
sherehe hizo yamefikia asilimia 50 hadi sasa. Amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa
Singida na kamati yake kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuhakikisha sherehe hizo
zinakuwa za mfano kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla. Singida Kuwa Kitovu cha Maadhimisho ya Mei
Mosi Kitaifa
0 Comments